Friday 13 September 2013

Padre amwagiwa tindikali huko Zanzibar

Padre Mwang'amba wa Kanisa Katoliki Zanzibar aliyemwagiwa tindikali huko Mlandege katika cafe ya Sun Shine. Tukio hilo limetokea katika cafe ya Sun Shine iliyopo maeneo ya Mlandege huko kisiwani Zanzibar...Padre huyo alifanyiwa kitendo hicho cha kinyama (kinyume na ubinaadamu) na watu wasiojulikani.

Matukio kama haya yamekuwa yakitokea mara kwa mara hapa nchini hususani huko kisiwani na kupelekea sababu sinazoleta mvunjiko wa amani hususani katika masuala ya kidini. Kama unakumbuka mwishoni mwa mwaka jana kuna tukio la kuuliwa Padre Mushi huko huko Zanzibar na watu wasiojulikana, pia mwezi mmoja kupita likatokea tukio la kupigwa risasi kwa Sheikhe (kiongozi wa kiislamu) pia na watu wasioweza kujulikana. Hii inadhihirisha kuwa matukio haya yanazidi kukua hapa nchini na kuleta mvunjiko wa amani.

No comments:

Post a Comment