Saturday 24 August 2013

Mupya ya kitaani leo hii

Katika pitapita zetu za leo tumekutana na hii mupya maeneo ya Kola - Makaburini, Morogoro tulipokwenda kumpumzisha " mzee Tandawala" Baba mzazi wa mdau wetu sana wa page na Blog yetu, Rasheed Tandawala "M/Mungu amrehemu". Mupya yetu ya leo ni pale tulipoona dingi mwenye miaaka kadhaa yaani kashatafuna chumvi za kutosha kama miaka 50 hivi imepita, ametupia kitu cha Tshirt yenye chata ya "GANJA". Hii ilitushangaza sana hasa vijana tunaojua ujana zaidi....

Kwa yeye sidhani kama alikuwa anajua zaidi ya kuona Tshirt imetulia mwilini na kuamua kujitupia tu kwa mwili pasipokujali nini kimeandikwa na maana ya maandishi hayo. Hatukatai kwamba waweza usijue maana ya maneno, hata picha jaman husielewe?? ebu tuwe wepesi wa kuchunguza kitu kabla hatujakitumia.




No comments: