Sunday 18 August 2013

M'bongo adakwa na madawa US

Jamaa wa Kibongo (mwenye asili kitanzania) aliyefahamika kwa jina la Joseph Mackubi amekamatwa huko Los Angeles airport (LAX), Marekani akiwa na madawa ya kulevya.

Mbongo huyo alidakwa akiwa ameficha madawa za kulevya aina ya Heroin ndani ya lap top. Yasemekana jamaa alipita kwenye zile screens za uchunguzi wa upitishaji wa mizigo halamu  pale airport , na wakahisi laptop ina kitu sababu ilikuwa nzito sana wakaitoa wakajaribu kuiwasha wakaona laptop ni mbovu haiwaki ndipo walipohisi kuna mchezo unaendelea hapo so wakaifungua wakakutaka na gram 800 za heroin.

Tanzania imekuwa inaongoza kwa sifa za kusafirisha madawa ya kulevya kwenye baadhi ya nchi kubwa hapa duniani, na hususani kwa mwaka huu report za kufanyika kwa bihashara hiyo halamu imezidi kuongezeka siku hadi siku...je tatizo liko wapi mbaka tunapoteza sifa nzuri kwa taifa hili lenye amani na utulivu kwa miaka mingi??

No comments: