Sunday 4 August 2013

Gervinho kuhamia AS Roma ya Italia

Staa wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Arsenal Gervinho yuko kwenye hatua za mwisho za kuihama klabu hiyo ambapo anakaribia kujiunga na As Roma ya Italia .
 
Gervinho tayari amefikia makubaliano binafsi na klabu hiyo huku Roma na Arsenal zikiwa kwenye hatua za mwisho za mazungumzo ya bei ya mchezaji huyo .
Gervinho alijiunga na Arsenal misimu miwili iliyopita akitokea Lille Metropole ya Ufaransa lakini ameshindwa kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza kwa muda wote aliokuwa na klabu hiyo ya London.

Kwa muda mrefu mchezaji huyo amejikuta akishindwa kuwa kipenzi cha mashabiki wa Arsenal kutokana na kuwa anakosa mabao mengi ya wazi awapo uwanjani hali inayofanya mashabiki kumzomea mara nyingi .
Cha kushangaza kuhusu Gervinho ni kwamba amekuwa akicheza vizuri akiwa na timu ya taifa na hata kufunga mabao muhimu tofauti na anapokuwa na Arsenal.

No comments: