Tuesday 16 July 2013

Shilole apata shavu USA

Mwanadada Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole, amejikuta kula shavu baada ya kwenda Marekani kupiga show kwa siku kadhaa na kubahatika kumkabidhi meneja wa mwanadada Jennipher Lopez maarufu kama JLo CD za kazi zake na meneja huyo kufanya kama alivyokusudiwa kwa kumpatia JLO apate kuzisikiliza ili aweze fanya nae kazi msanii huyo.
''Meneja wa Jennifer Lopez alimpatia Jennifer Lopez CD zangu... Kasema amenikubali na nikirudi tena Marekani baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, tutaonana''...alisema Shilole

Sisi kama wadau wa muziki wako na pia watanzania wenzio tunakutakia kila la kheri bidada Shilole.

No comments:

Post a Comment