Saturday 27 July 2013

Nando na Feza wamteta Elikem

Hali hii imetokea baada ya tukio lililotokea jana usiku Julai 27, ambapo washiriki wa Jumba la BBA "Nando na Elikem" kuzinguana.
Hivyo leo wakakutana chemba Watanzania hao "Feza na Nando" nakuanza kumteta Mghana huyo "Elikem"...
"Kila siku huwa nasema ukweli," Nando alimwambia Feza huku Feza akionesha kumsapoti..."kweli umefanya kile ambacho wengi wanashindwa kusema ukweli"...huku Nando akitikisa kichwa kuonesha wanaelewana sawasawa. "Wale jamaa Elikem na Cleo, bila shaka wana kitu" Nando aliongeza.

Watanzania hao wakaendelea kutia jungu kwa kumkashifu kuwa jamaa bado hajakua..."Anaongea kama mtu anaekua" Nando alisema. "Kweli hajakuwa bado, na huna sababu ya kuendelea kuongea na mtu ambaye hajakuwa bado" Feza alimueleza Nando. Nando alimsapoti..."Yah najua"...."Na ndio maana anajichanganya mwenyewe" Nando alisema.

Tuzidi kuendelea kuifuatilia ishu iyo tutawapa yanayojili kwenye Jumba hilo la BBA.

No comments:

Post a Comment