Mwanajeshi
anayesadikiwa kukutwa na jino la
Tembo akiwa chini ya ulinzi pamoja na
kidhibiti
OFISA Uvuvi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Suleiman Chesana,
anayekabiliwa na kesi ya kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh
bilioni nne, amepandishwa kizimbani baada ya kukutwa na meno
mengine ya tembo kilo 781 yenye thamani ya Sh bilioni 9.3. Mshtakiwa huyo, alipandishwa tena kizimbani jana kwa mara nyingine
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mjini Dar es Salaam, mbele
ya Hakimu Sundi Fimbo na kusomewa mashtaka na Wakili Mwandamizi wa
Serikali, Tumaini Kweka. Kweka alidai kosa la kwanza ni la kujishughulisha na nyara za Serikali bila kibali, kinyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi. Ilidaiwa Mei 23, mwaka huu, katika mpaka wa Malawi na Tanzania,
mtuhumiwa alikamatwa akisafirisha isivyo halali nyara zenye thamani ya
Sh bilioni 9.3, zikiwa zimefichwa katika mifuko ya saruji, wakidai
wanasafirisha saruji.
No comments:
Post a Comment