
Mwanamuziki Linah Sanga amezikanusha ripoti
zilizosambazwa leo kuwa amebakwa na rapper Kimbunga na kudai kuwa
ameshangazwa mno na taarifa hizo. Taarifa hizo zimeanza kusambazwa leo mchana baada ya akaunti ya Facebook
inayoonekana kuwa ya rapper Kalapina yenye jina ‘KalApina Kikosi Cha
Mizinga’ kuandika....“Mtoto kimbunga amechamba ana leta usela
mavi mambo ya kizamani hivi yupo chini ya ulinzi osterbay police kwa
kosa la kumbaka msanii lina.”
Bongo5 imezungumza na Linah
ambaye amesema amepigiwa simu na watu wengi wa karibu kumuuliza suala
hilo wakiwemo, Barnaba, Ditto, Amini na mtangazaji wa Clouds FM, Soudy
Brown.Amesema Soudy alimwambia kuwa ameziona taarifa hizo kwenye Facebook kwenye akaunti ya Kalapina.
“Sasa nikasema Kalapina ameandika hivi, kwasababu sijaingia mwenyewe
kuangalia chochote. Sikutaka kujipa stress kwasababu kuna kazi nafanya
nisije nikaharibu kazi kwahiyo nikaona vitu vingine kama hivi ni vya
kupotezea tu lakini sio vizuri kabisa yaani. Kiukweli sijapenda, yaani
bora mtu anizushie kitu kingine chochote lakini si suala kama hilo hapo,
si suala zuri,” amesema Linah.Amesema jana usiku alitoka na mpenzi wake kwenda kwenye sinema na wakarejea nyumbani salama.
“Sasa sielewi huko kubakwa nimebakwa saa ngapi na nilikuwa na boyfriend
wangu labda yeye ndio kanibaka! Maana mtu wanayeniambia amenibaka
Kimbunga, huyo Kimbunga hata simjui, namskia tu.Nashindwa kuelewa,
kwanini mtu azushe kitu kama hicho yaani ndo nataka kujua source ni
nini.
Niko fine yaani, kwasababu naelewa ‘it’s not true, lakini
nafikiria huyo mtu mpaka kaamua kunifanyia kitu kama hicho, nimemkosea
nini au kuna kitu gani, yaani hicho ndio kinaniumiza kichwa.”
No comments:
Post a Comment