Jamaa aliyefahamika kwa jina la Wati Holmwood, mwenye umri wa miaka 33, mwenyeji wa Sydney aliamua kuingia ndani ya uwanja
wa ANZ na kuanza kucheza huku akiwa uchi kama alivyozaliwa.

Jamaa
huyo mwenye mwili kiasi cha kutosha alikimbizwa na kudakwa na walinzi
katka kile kilichochukua muda wa dakika kama moja kuuzunguka uwanjani.
Holmwood alisema alitaka kukimbia umbali wa kilometa 10 akiwa kwenye hali hiyo mara baada ya kutolewa nje ya uwanja.

Inafahamika
kwamba Holmwood aliupaka mwili wake mafuta ili kuwe na
ugumu wa kumshika pale atakapokamatwa na vyombo husika akiwa kwenye
zoezi hilo.

Juhudi
zake zilimkuta akiishia hospitali ya Auburn iliyopo ndani ya jiji la
Sydney huku gazeti la Telegraph likitaarifu alionekana akiwa
"amechanganyikiwa na hajielewi" baada ya kuamka na kujikuta kwenye hali
aliyokuwa nayo.
No comments:
Post a Comment