
Dayna akiweka Mshumaa juu ya Kabuli
Mwimbaji wa nyimbo za mafungu ya nyanya, Fimbo ya mapenzi, Nivute
kwako na ule unaotamba sasa wa Leo, Dayna Nyange mkali wao, ndani ya
mwezi mtukufu, amefanya ziara ya kumkumbumbuka na kutembelea kaburi
alilozikwa mwanamuziki mwenzie toka Morogoro, Albert Mangwea
Dayna ameonekana katika kabuli la Mangwea, mwanzoni mwa mwezi huu
mtukufu wa Ramadhani. Akizungumza na mwandishi wa Habari hii mara baada
ya tukio, Dayna amesema Albert Mangwea ni mmoja ya wasanii aliokuwa
nao karibu sana na alikuwa akimsaidia kwa mambo mengi sna katika mziki
"Unajua Albert Mangwea ni zaidi ya msanii mwenzangu, alikuwa kama
ndugu kwangu. Albart alikuwa akinishauli mambo mengi sana juu ya mzikim
na hata maisha pia. Hivyo ni wajibu kwangu kumkumbuka mara kwa mara.
Pia kitu ambacho hukijui, Ngwea ni mmoja ya wasanii walionisaidia sana
hasa kusambaza wimbo wangu huu wa sasa nilioimba na Mr: Blue - Leo.
sitamsahau my Brother Ngwea na ndiyo maana ndani ya mwezi mtukufu
nimetenga siku ya leo kuja kumtembelea. Pumzika kwa amani japo pengo
lako bado lipo'' Amemaliza huku akibubujikwa na machozi.
Dayna akipiga saluti ishara ya kumkubali Marehemu Albert Mangwea
Pumzika kwa amani Ngwae.
SHUKRANI KWA CHANZO CHA HABARI HII: AHMAD MACHAKU
No comments:
Post a Comment