Aliyekuwa
mgombea UWT Taifa, Maryrose Magige akionyesha kadi ya Chadema
aliyokabidhiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa wakati wa
mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi
Manzese Dar es Salaam.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimedai kunasa waraka wa
siri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaokwenda kwa Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Mpya, Jaji Joseph Warioba, ukimshinikiza kukubali
mapendekezo yao.
Waraka huo wa CCM uliosainiwa na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini,
Jitu Vrajilal Soni una lengo la kupinga mapendekezo mbalimbali yaliyomo
katika Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba Mpya iliyozinduliwa Juni 3 mwaka
huu.
Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Mashariki na Pwani, Mabere Marando
akihutubia mkutano wa chama hicho uliofanyika katika viwanja cha Shule
ya Msingi Ukombozi, Manzese jijini jana alidai waraka huo una lengo la
kuvuruga mchakato wa kupata Katiba Mpya yenye manufaa kwa Watanzania
wote.
Marando akisoma baadhi ya mapendekezo ya CCM yaliyomo katika waraka
huo kwenda kwa Jaji Warioba kumtaka kuviondoa vipengele vilivyomo ndani
ya Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba Mpya vinavyohusu Tunu ya Taifa, kuwa
bila kufanya hivyo hakutakuwa na tija ya uwajibikaji.Kusoma zaidi bofya
Alizitaja tunu hizo za taifa kuwa ni kuwa utu, uzalendo, uadilifu,
umoja, uwazi, uwajibikaji na lugha ya Taifa ambazo Chadema wanaziunga
mkono zipite na kuwa sheria.
“Sisi Chadema tunaona zinafaa kutokana na umuhimu wake lakini CCM
wamemwambia Warioba aondoe neno uwazi wakiwa na maana ya kuwa wanataka
mambo yao yasiwekwe wazi,” alisema Marando.
Marando ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho alisema,
Jaji Warioba amependekeza utajiri wa taifa uendelezwe na kuzuia mtu
kumnyonya mwenzake jambo ambalo CCM wamelipinga.
“CCM katika waraka huo ibara ya 11.2 na 11.3 wamemwambia Warioba
viondolewe, sasa viongozi wa CCM na Chadema ni kina nani wanawapenda
wananchi wake,” aliwauliza wananchi waliojitokeza katika mkutano huo na
kujibiwa na kelele kuwa ni Chadema.
Marando alisema katika kipengele cha maadili ya taifa na jamii
kinachosema viongozi wanatakiwa kuzingatia uongozi, utoaji wa huduma,
kufanya usawa na kupiga vita rushwa mapendekezo ambayo yakipita kuwa
sheria yatasaidia kupunguza tatizo la rushwa la utoaji wa huduma
uliotukuta.
“CCM ambao hawaonyeshi dhamira ya kumkomboa mwananchi wake,
wamemwambia Warioba kuyaondoa maadili hayo kwani hayafai, sasa kupiga
watu, kula rushwa kweli liondolewe? Hawa CCM kweli hawataki tupate
katiba ya kuwakomboa wananchi,” alisema Marando na kuongeza:
“Kama hiyo haitoshi wamesema kitendo cha wananchi kumwajibisha mbunge
wao kama hatakuwa anatimiza majukumu yake nao wamesema mapendekezo hayo
hayafai. Kweli CCM hawataki tupate Katiba Mpya.”
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
No comments:
Post a Comment