Monday, 13 May 2013

Zitto aampa Afande Selle dollar 1000 akashoot video

Mfalme wa Rhymes Selemani Msindi a.k.a Afande Sele wakati alipo hudhuria kwenye uzinduzi wa msimu mpa wa Clouds fm ulioenda sawa na semina kuhamasisha vijana kujitambua kwa kutumia fursa za kiuchumi zilizopo nchini, Lakini pia kulikua na uzinduzi wa kampeni kubwa ya kupinga Uharamia wa kazi za kisanii / Anti Piracy, Afande alibahatika kupata ahadi ya dola elfu moja kutoka mbunge wa kigoma kaskazini Zito Kabwe, mh zito alisema anatoa kiasi hicho cha pesa ili afande aka shoot musiq video ya ngoma yake aliyoitoa hivi karibuni inaitwa "Dini tumeletewa" Mbunge Zito Kabwe amesema kutokana na ubora wa ngoma hiyo anatoa mchango huo ili ikafanyike video bora itakayodumu muda mrefu na kuwafikia watu wengi, ili ikawa elimishe watanzania na vijana kwa ujumla umuhimu wa kupendana na kuacha kubaguana katika misingi ya dini.
Ngoma hii "Dini tumeletewa" imekuja baada Kutokea mauaji ya viongozi wa dini pamoja na shambulizi la bomu lililofanywa hivi karibuni katika kanisa moja huko Arusha na kuua watu kadhaa.

zaidi Sikiliza sauti Afande akifunguka kuhusu ishu hiyo:
Isikilize ngoma yenyewe hii hapa:

No comments: