Wednesday 8 May 2013

Prezzo afunguka mara ya kwanza baada ya kifo cha Goldie

Mshindi namba mbili wa shindano la Big Brother Afrika 2012 ambae alikua anatarajia kumuoa Marehemu Goldie mwaka huu, CMB Prezzo, amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya ukimya uliotokana na msiba wa mpenzi wake Mnigeria Goldie.

CMB ambae ameyaongea hayo wakati amekuja kufanya show yake ya kwanza Tanzania tangu kutokea kwa kifo cha Goldie, amesema siku ya msiba February 14, 2013 ndio ilikua mara yake ya mwisho kuongea na Goldie...
Alikua Nairobi kwenye ndege akikaribia kupaa kwenda Nigeria, neno la mwisho Goldie alilomwambia ni kwamba alikua kwenye internet akitafuta kujua jinsi ya kupika pilau, wale pamoja akifika Lagos Nigeria.
Alipofika Nigeria hakupokelewa kama ilivyokawaida, hakukua na mtu yeyote Airport.. kumbe saa moja iliyopita ndio Goldie alifariki, Prezzo akiwa palepale Airport alijaribu kupiga simu ya Goldie na haikupatikana lakini mama yake mkubwa akaongea na Prezzo kwamba ameshafariki.
Prezzo ambae amesema Valentine’s day haitakua nzuri milele maishani mwake, baada ya kifo cha Goldie, alikaa Nigeria kwa wiki mbili na ilibidi aondoke kabla ya maziko kutokana na mfarakano uliotokea ambao hakupenda kuuingilia ila ameahidi kwenda kulitembelea kaburi muda wowote kutoka sasa.
Prezzo alikuwa Tanzania ambako jumamosi May 4 2013 alifanya show Grand Regency Hotel...

No comments:

Post a Comment