Thursday 9 May 2013

Patcho atokewa na mzimu wa Kanumba

Mwigizaji wa filamu za kibongo na pia mwanamuziki wa Dansi Patcho Mwamba aliyekuwa karibu sana na aliyekuwa nguli wa sanaa ya filamu na maigizo nchini, marehemu Steven Charles Kanumba amesema kuwa kuna wakati anatokewa na marehemu Kanumba akiwa amelala na kumwita huku akimsihi kusema mema na kuwa na upendo katika jamii maana anaamini kuwa Duniani maovu yamezidi na kitu kikubwa ni wasanii hawapendani, chuki, wivu vimetawala kwao.

No comments: