Thursday 2 May 2013

Kweli nimeamini kufa kufaana

Kwa taarifa zilizotufikia ni kwamba jana kulitokea ajali mbaya ya basi katika maeneo ya Chalinze nje kidogo ya jiji la Dar es salaam ambapo basi na lori yaligongana, hata hivyo hakuna taarifa za kifo cha abiria yeyote zaidi ya kuwepo kwa baadhi ya majerui.
.
.
Kondakta wa basi ndio huyu ambae aliteguka kiuno ambapo kuna mama ambae mguu wake ulikatika.
Hizi ni baadhi ya picha za ajali hiyo
Sasa kwa ule msemo wa kiswahili au wahenga waliosema kuwa "kufa kufaana" umedhihirishwa jana baada ya kuwepo kwa vijana wawili waliokuwepo eneo la tukio na kufanya kitendo ambacho si cha kiubinadamu kabisa, baadala ya kuwasaidia majerui wa ajali hiyo wao wakataka kuwaibia ndipo wakadakwa na watu wa usalama na kuwekwa chini ya ulinzi....
Ivi Tanzania utu umepotea kiasi hiki?? na wapi tunakoelekea sasa kama hali inazidi kuwa tete.

No comments: