Thursday 2 May 2013

Alichosema Gadna kuhusu Jay Dee kuacha wosia

Baada ya Lady Jay Dee jana 1, May kufunguka yake ya moyoni kuhusu Luge na Kusaga na kuamua kutoa wosia endapo ikatokea yeye hayupo tena duniani.
Gadna ambaye ni mume wa Lady Jay Dee amefunguka kuhusu ishu hiyo wakati akiongea na mtangazaji wa TBC FM Dan Chibo. 
NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA:

Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?
Gadna G: Ni maneno  ambayo yametoka moyoni mwake na  ni maneno  mbayo anajiteteakama msanii,  mimi kama Meneja ukiacha pia kama  mke wangu naendelea kumsapot kwa kile ambacho anaona ni sawa, basi mimi nitaendelea kumsaport  na kujaribu kuzungumza naLady Jay Dee, mara nyingi anasema tu kwamba  watu wasifikilie ni swala la wimbo kupigwa au kutokupigwa, hayo ni mambo ya kawaida lakini wafikirie tu kwamba huyu mtu anaongeakutokana experience yake aliyokuwa nayo na wale watu. Baada ya mwaka 2003 kuacha kufanya kazi kwenye management yao ya Smooth Vibe, yalitokea mambo mengi hapa katikati  ila hakusema lakini siku za hivi siku za karibuni kuna mengine ambayo yametokea, ndio akaona hapana nisipo sema nitazidi kukandamizwa na matokeo yake nitakufa kisabuni.

Hii ni kama vita mmejipangaje..?
Gadna G: Unapoamua kusema ukweli swala la kujipanga mara mbili huwa halipo, ni kwamba unasema ukweli watu wasikie  naukizungumzia uhasama watu watauliza juu ya uhasama  lakini ulikuwepo tayari kwahiyo tu watu wanajua kwa sasa kwa kuwa jdee ameamuwa kuongea lakini tu hawajui tu kwamba jdee alikuwa na matatizo na wale watu tangu kipindi cha nyuma sababu wale watu wanafumo dume ya kufanya kazi na alipoachananao aliona kama wanamfatilia  kulekule ambapo yeye alipo 

Nini mlikiona kama chokochoko...?
Gadna G: Unajua kwa mfano unaweza kumuomba mtu maji akakwambia sina, ukayaona yale  pale ukamwambia niuzie akakuuzia ila bado alivyokuuzia  akaona kama unafaidi, mwisho  akakwambia yameisha nenda sehemu nyingine, ukaenda sehemu nyingine na ukayapata bure, akaona umepata akaamua kukufata kulekule na akakukuta unakunywa maji kwenye grasi kisha akakuputa, sasa hapo inabidi useme hapa unavyofanya sio sawa ndo hicho anachofanya Jay Dee sasa hivi.

Hali hii imewaathiri kwa kiasi gani...?
Gadna G: Cha kushukuru Mungu ni  kwamba msanii au hata pia stesheni ya redio inategamea umma wa Watanzania au  hata mashabiki kwa ujumla kwa kuwepo kwake.
Jay Dee anapata saport nzuri kutoka  Watanzania, basi ujue hata hajaathirika chochote, na pia tu anaendelea kufanya kazi kwa bidii, ila tu isipokuwa unapoona mtu anafanya madhara ili tu mtu apate athari fulani ndio unasimama kuongea, ndiyo maana tuna Bunge na watu wanasimama, watu wanaongea, watu wanatetea hoja, ndiyo maana yake. Yani lazima mtu usimame useme ukweli kwa unalohisi hili jambo litanipa madhara nisiposema.

Kwa Wasanii wengine unawaambiaje...?
Gadna G: Uwoga ni kitu ambacho binadamu tumeumbiwa, wakati mwingine unasaidia wakati mwingine unakudhiru uwoga wako,kwa sababu wanasema adui wa maendeleo yako mwenyewe ni wewe mwenyewe, ndiyo maana uwoga wako unaeza ukasabishwa ukakandamizwa zaidi, ndiyo maana wazee wetu waliweza kusimama na kuikomboa hii nchi kwa sababu walisimama hawakuogopa. Wangeogopa hii leo hii nchitusingekuwa huru, kwa hiyo kama kuna mtu ana jambo na anaogopa kusema hilo ni jambo la kawaida kuogopa,lakini wakati wa kusema ukifika usiogope kusema ili mradi useme ukweli, basi inatosha....

Kauli yako ya mwisho ni ipi..?
Gadna G: Ni kwamba wanahitaji kujua ukweli na kuambiwa ukweli, mtu yoyote anayejua kitu cha kweli anaweza kusema sio sawa, utaendelea kukandamizwa. Kauli ya mwisho  ndo hiyo wanahitaji kuambiwa ukweli na  kusikia ukweli  ili kama wanakosea wasiendelee kukosea  wabadilikee….

No comments:

Post a Comment