Tuesday 30 April 2013

Smartphone yabuniwa kwa matumizi ya vipofu

Kwa kile ambacho kimedaiwa kuwa ni moja ya ishara ya kudhihirisha kuwa teknolojia inazidi kukua duniani ni baada ya wanateknolojia duniani kutengeneza Smartphone ambayo itatumika kwa msaada wa watu wenye matatizo wa macho (upofu). Idea ya teknolojia hii ilianza kufikiriwa tangu mwaka 2011 na mwanateknolojia wa India aliyesoma chuo cha NID (National Institute of Design) aliyefahamika kwa jina la Sumit Dagar.
Sumit Dagar amefikiria kuwepo kwa teknolojia hiyo ya Smartphone ili kuwasaidia baadhi ya watu wenye matatizo hayo ya kuona(upofu). Hata hivyo Smartphone hiyo haijapewa jina kamili mbaka hivi sasa na inamatumizi tofauti na Smartphone zingine, kwa kuwa itakuwa na grid pins ambazo zitakuwa zina'move up and down kwa kusaidia walemavu hao kuweza kusoma/kuandika/kupokea SMS au Emails. Itakuwa inatumia teknolojia iitwayo Shape Memory Alloy itakayozifanya pin hizo kutanuka, kuacha kumbukumbu na kurudi kwenye umbo lake la kawaida.
Kwenye mahojiano na moja ya kituo cha habari cha nchini India kiitwacho Times, Dagar ameielezea simu hiyo ambayo itakuwa ya kwanza duniani kote kwa matumizi ya vipofu, amesema wazo hilo alianza kulifikiria takribani miaka mitatu sasa ambapo aliamua kushirikiana na baadhi ya wanateknolojia wenzie wa IT Delhi wa huko nchini India, pia amesema teknolojia hiyo wameshaipeleka kwenye Taasisi ya macho ijulikanayo kama "LV Prasad Eye Institute" Dagar na wanateknolojia wenzake wamepanga kuiachia simu hiyo mwishoni mwa mwaka huu (2013).

No comments:

Post a Comment