Monday 29 April 2013

Tetesi ya Justine Bieber na Selena Gomez kurudiana

Baada ya kuwa nje ya mahusiano ya kimapenzi wawili hao (Bieber na Selena) kwa kipindi cha muda sasa, wameanza kuonesha ishara ya kurudisha penzi hilo moto moto lililoshamiri kwa kipindi kile wanaanza mahusiano yao.

Mapema wiki hii zimevuma kuwa wawili hao watakuwa wamerudisha hisia zao na kuamua kuwa pamoja japo haijawa wazi. Mapaparazzi wamefuatilia mpaka wamepata uhakika kwamba mwimbaji Justine Bieber na mpenzi wake Selena Gomez wamerudiana... Mpango huo wa kurudiana ulithibitika wakati Bieber yuko Norway akifanya show, Selena naye alimfuata…. Pirikapirika zao ndio zilifanya mkanda mzima upatikane ikiwemo Selena kuandika kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii kama facebook na Twitter...
Alichopost Jumamosi usiku kupitia
mtandao wa instagram
(Pichani)Justin Bieber alipopigwa picha akiwa 
amesave picha ya Selena kwenye wallpaper

No comments:

Post a Comment