Thursday 11 April 2013

alichosema uwoya juu ya skendo yake na diamond

Baada ya habari nyingi sana kuhusu Irene Uwoya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Diamond Platnumz kutawala baadhi ya vyombo vya habari hususan magazeti ya udaku na kwenye mitandao ya kijamii hapo juzi, hatimaye baadhi ya waandishi wa habari waliamua kumtafuta kwa simu mwanadada Irene Uwoya ili waweze kumuuliza juu ya tuhuma hizi za yeye kuingilia penzi la mwanadada Penny kwa kijana Diamond Platnumz…
Baada ya majaribio mengi ya kupiga simu yake ambayo ilikuwa haipatikani muda wote, hatimaye waandishi hao waliweza kumpata hewani na jibu lake lilikuwa moja tu kuwa : “ACHANA NAZO!!!” halafu akakata simu… Na waandishi hao wakaona kweli waachane nazo ila wawafikishie nyie wasomaji jibu hilo la Uwoya ili wenyewe muamue na kutafakari… Hilo ndio jibu alilowapa mwanadada mrembo wa bongo movie, Irene Uwoya kuhusu tuhuma za yeye kutoka kimapenzi na msanii Diamond…
Tafakari mwenyewe!...

1 comment:

Anonymous said...

Hello there! This post couldn't be written any better! Reading through this post reminds me of my old room mate! He always kept chatting about this. I will forward this post to him. Fairly certain he will have a good read. Many thanks for sharing!

my web page - http://paydayloanspup.co.uk/