Ilikuwa gari aina ya Harrier ni IT kwa maana ni mpya iliyokuwa ikipelekwa Tunduma kutokea Dar es salaam kwa mnunuzi. Kama ilivyoada kwa madereva lazima wadake vichwa njiani, basi dereva ikabidi adake vichwa vyake vinne (4) hivyo gari ikawa na watu watano na miongoni mwao alikuwepo mdogo wangu aliyekuwa akielekea Iringa baada ya kukosa basi stand ya Ubungo.
kufika morogoro maeneo ya sangasanga gari ikiwa kwenye speed ya 160 ikatokea bodaboda dereva akiwa anayumba, dereva wa Harrier ikabidi amkwepe ghafla wakataka kukutana na Semi mbele likiwa kwenye mwendo kasi, ikabidi waache nji na kuingia porini ili kukwepa kugongana uso kwa uso na semi. Ghafla gari ikaanza ku'roll ikageuka mara sita. hapo hapo dereva agapasuka sehemu ya kichwa na mgongoni, jamaa aliyekaa nyuma ameumia mkono, cha ajabu dogo wangu aliyekuwa amekaa mbele hakuumia hata kidogo zaidi ya kuumia sehemu ya kidole tu na wale jamaa wawili waliokaa nyuma nao wametoka salama salimini.
Mungu mkubwa na wakushukuriwa sana kwa kuponya maisha ya ndugu yangu na jamaa waliokuwepo kwenye gari hilo.
Mungu mkubwa na wakushukuriwa sana kwa kuponya maisha ya ndugu yangu na jamaa waliokuwepo kwenye gari hilo.
gari kabla ya kupata ajali
damu iliyoachwa na dereva
hapa ndipo alipoumia dogo...mungu yunawe
No comments:
Post a Comment