Sunday, 28 October 2012

je ni kweli shule ufanya maisha yawe na safari ndefu sana?

Watoto wenye umri chini ya miaka 7 wakienda shule iliyo umbali wa kilometa 2 wakiwa na vitendea kazi vinavyowalazimu kuwa navyo kila siku waendapo shule
Huyu nae anasoma mbali na anapoishi kwahiyo umlazimu kuomba rift kwenye usafiri huu (Guta) ili awazekuwahi shule

Kwa wale waliosoma miaka ya 1990's au 1980's wanaweza kusimulia maisha yao ya shule kwa mtazamo uliotofauti kabisa na wale tuliosoma miaka ya 2000's. Kwa ujumla maisha ya shule ndio yanabeba asilimia kubwa sana katika maisha ya kila mwanadamu kwa kuwa takribani 80% ya maisha unaitwa mwanafunzi. Nikisema mwanafunzi namaanisha maisha yote yale yawe ya shule ya msingi, sekondari au chuo kikuu, pia nawajumuisha na wale waliosoma/wanaosoma ufundi wa aina yoyote ile. Hivyo basi kwa kuwa shule ndio inayobeba asilimia kubwa sana ya maisha yetu ya kila siku, kuna vikwazo, vishawishi,  vipingamizi vingi sana ambavyo vinatufanya tuyaone maisha mazuri au mabaya kwa mitazamo yetu tofauti.

Wapo wanaoona shule inawafanya wayaone maisha ni magumu kwa pilika za adhabu, kusumbuliwa na walimu (kutongozwa), kurudia mitihani (kufeli), kutembea umbali mrefu na pia wapo wanaoona shule inawapa furaha ya maisha yao kwa kuona mafanikio yanayowezesha kuendesha maisha katika furaha sana, kwa mfano; wapo wanaopata wachumba shuleni kisha wakapata furaha, wapo wanaopata ajira wakiwa shuleni, wapo wanaoheshimiwa na kuthaminiwa kwa kuwa wapo shuleni, pia wapo wanawanyanyasa wenzao kwa maslai yao kwa kuwa tu wapo shuleni/wanasoma shule. kwa mitazamo hii yote inayoshabihana kwa namna moja au nyingine ndio uijenga au kuibomoa safari ya maisha yetu na kuiona kuwa ina mambo mengi saana.

Kwa mtazamo nilionao, najiuliza ivi kusingekuwa na maisha ya shule kungekuwa na safari ndefu kama tulionayo au kuipitia kama hii tunayokabiliana nayo hivi sasa??

No comments: