Friday, 20 January 2012

YALIYOJILI KWENYE MSIBA WA MH. REGIA MTEMA

Marehem Regia Mtema
Ni taarifa nilizopewa na mwanaharakati aliyekuwepo kwenye shughuli nzima ya msiba wa Mh. Regia Mtema aliyefariki dunia January 15,2012.
Bwana Aziz Himbuka alisema: 
"niliyoyashuhudia ifakara wakati wa mazishi ya regia mtema. kwa kuanza ni msafara mrefu ulikua na magari zaidi ya 30. tulipokaribia maeneo ya kaporo muda wa saa mbili usiku tulikuta watu wengi wakiwa wamejitanda barabarani wakiwa na uso wenye huzuni na mara 2lipofka kibaoni inapoanza lami tulikutana na kundi la watu la vijana, wakinamama, na wazee wakiwa wamelala barabarani kwa kutaka msafara usiende kasi na badala yake uende polepole kwa wao kuusindikiza kwa miguu. baada ya askali kutaka kuzuia kwa madai wamechoka lkn kutoka na uwingi wa watu waliojitokeza, nguvu ya umma ndio iliyofanikiwa, na msafara uliendelea kwa kusindikizwa kwa miguu, wengine wakiwa na baiskeli na bodaboda za kutosha. watu walijitokeza kwa wingi sana na hii kwa historia ya kilombero haijawahi kutokea japo walitangulia wabunge kama marehemu Guramali, kiwanga na watu maarufu wengine. ulikua ni umbali wa km5 kutoka kibaoni hadi ifakara mjini ambapo ndipo msiba ulipokuwepo. tulifika nyumbani muda wa saa 4 na watu walikua ni wengi haijawatokea. kutokana na uwingi wa watu iliamuliwa kuwa siku ya kuaga mwili itabidi upelekwe eneo la wazi (uwanjani) na ndipo ulipopelekwa katika kiwanja cha kiungani na hapo watu waliendelea kujitokeza kwa wingi japo mvua ilinyesha lakini watu waliendelea na shughuli ya kuuaga mwili kama ilivyopangwa. na muda wa maziko watu waliuzindikiza mwili hadi kwenye makabuli ya kwa mkuya. na hatua za mazishi zilifuata kama kawaida. matukio baada ya mazishi, mbunge wa kilombero Abdul Mteketa alizomewa na wananchi na kuonyeshwa alama ya vidole viwili. na mara walipomuona dr. slaa wananchi walimshangilia na kuanza kusukuma gari lake huku wakiimba 'rais rais rais rais'. kusema kweli marehemu regia alipendwa na wanakilombero. na hii ni kutokana kuwa karibu na wananchi wake. nilichojifunza kutoka kwake ni kujituma".

No comments: