Ni miongoni mwa kundi ambalo lilishika na kuteka takribani
Tanzania nzima na nje ya Tanzania kupitia kibao chao
cha kamanda, nyimbo ambayo ilikuwa na
mtazamo wa kuuzunisha na kutia majonzi kupita
kiasi, pia ni nyimbo ambayo iliongoza
kwa kuandikwa sana kwenye magazeti takribani
yote ya Tanzania, mbali na hilo pia iliongoza
kwa kukaririwa kimashahiri na kila mtanzania,
mbali na Kamanda, Daz Nundaz walibamba
na vibao kama Maji ya shingo, Barua, Nitafanya
na vingine vingi vilivyomo kwenye Album yao
iliyopewa jina la KAMANDA.
Ila mwanzoni mwa mwaka 2005 kundi
likasambaratika na kila mtu akaanza fanya
kazi kama solo artist, ndipo Ferouz, Daz Baba
wakajipanga na kila mtu kudondosha Album
yake, Ferouz alianza na Album ya Safari
akafuatia Daz Baba na WIFE na kuwaacha
wanakundi wengine kufa kabisa kimuziki.
Kiukweli kwa miaka ya hivi karibuni jamaa game
imewashinda kabisa na kujikuta wanachemka kila
wakitoa ngoma inakuwa kapuni. Mwanzoni mwa
mwaka 2011 ilifahamika kuwa kuna mwanakundi
mmoja wa Daz Nundaz "Sajo" amepoteza maisha.
Mungu amlaze mahali pema peponi..Amen!!
Kwa mtazamo wangu, sidhani kama jamaa
wataweza rudi tena kwa jinsi game ilivyo kwasasa
No comments:
Post a Comment