Saturday, 14 January 2012

R.I.P MH. REGIA ESTELATUS MTEMA


Mbunge wa viti maalumu Kilombero (Chadema), Mh Regia Estelatus Mtema amefariki dunia mapema jana asubuhi mnamo majira ya saa 5 ktk ajali mbaya iliyotokea maeneo ya Ruvu, Mkoa a Pwani, kwa ajali ya gari.
Aidha imeelezwa kuwa Mbunge huyo wa Viti Maalum umemkuta umauti wakati akielekea kukagua Kiwanja alichopewa na Wazazi wake kama zawadi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, ni kuwa gari ya mheshimiwa haikugongana na gari yoyote ila ilipotea njia wakati kitaka ku-overtake gari nyingine na kupoteza muelekeo ikapinduka mara tatu na kuingia porini.
Majeruhi waliokuwa kwenye gari akiwemo mama yake mzazi ni; Roger abdallah, Paulina, Simon, Bernedeta, Peter na Lawrence.

Muonekano wa gari alilopata nalo ajali kwa nyuma
 Muonekano kwa mbele
Upumzike kwa amani rafiki, Dada na kiongozi wetu mpendwa umeondoka katika kipindi ambacho Tanzania inakuhitaji hasa....
Pole kwa familia, Pole kwa CHADEMA, Pole kwa vijana wote wa Tanzania, Pole kwa wana Kilombero, Pole kwa watanzania kwa jumla. Hakika hili ni PIGO kwa watanzania.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen!!

No comments: