BELLE IX
Msanii wa bongofleva, Abelinago Damian alimaarufu kama Belle 9,
leo ameviambia vyombo vya habari kuwa mashabiki na
wapenzi wake wakae mkao wa kula kwa ngoma "nyimbo"
yake ambayo anatarajia kuiachia kesho. Ngoma hiyo aliyoipa
jina la AMERUDI ameifanya peke yake bila kumshirikisha
msanii yoyote yule.
Belle 9 aliyetamba na ngoma kadhaa kipindi cha nyuma
kama Sumu ya Penzi, Masogange, Wewe ni wangu aliyofanya
na Blue, pia Nilipe nisepe ambayo ndio nyimbo yake
ya mwisho kuiachia, imempa show nyingi sana kwa mwa 2011.
Anatarajia mtaipokea vizuri na kuipenda sana,
kifupi ni muendelezo wa masogange..
kwa zaidi subiri kesho uisikie hiyo ngoma,
nikiipata nitaitupia muweze isikiliza
No comments:
Post a Comment