Mvua iliyoanza kunyesha tangu juzi tarehe 19,
imeacha vilio kwa wakazi wa jiji la Dar- es-salaam
baada ya kuharibu nyumba, magari, na mali mbalimbali.
Pia imeleta vifo vya watu hadi sasa takribani 17,
ambapo juzi ilirepotiwa na vyombo vya habari kuwa
watu zaidi ya watano (5) wamepoteza maisha
baada ya wawili kusombwa na maji, mmoja
kupigwa na radi na wawili kupigwa shoti baada
ya nguzo ya umeme kugusa maji na kusababisha shoti.
Hivi sasa jiji limegubikwa na majonzi makubwa baada
ya wakazi wengi hasa wale wa mabondeni kukumbwa na mahafa hayo.
Hii inarepotiwa kuwa mvua yenye kuambatana na radi na
upepo mkali kama hii inayoendelea kunyesha jijini
Dar -es -salaa iliwahi kutokea miaka ya 1960's na kuharibu mali nyingi sana.
Hadi sasa serikali halijatoa tamko lolote kuhusiana na tukio hilo.
Gari la zimamoto la kituo cha uwanja wa ndege
@Kigogo mbuyuni
@Mwananyamala
kigogo darajani karibu na Shule ya msingi ya Gilman rutihinda
TAARIFA KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIAKutokana na ongezeko la mvua zinazoendelea katika maeneo mengi nchini Mamlaka ya Hali ya Hewa inatoa taarifa ya mwelekeo wa mvua hizo katika kipindi cha siku kumi zijazo kuelekea mwaka mpya 2012.
Mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuimarika kwa hali ya joto la Bahari ya Hindi, sambamba na kuongezeka kwa msukumo wa hewa yenye unyevunyevu kutoka misitu ya Kongo na kusababisha makutano ya upepo katika eneo la mashariki na kusini magharibi mwa nchi.
Hali hii inatarajiwa kuendelea kusababisha vipindi vya mvua kubwa katika maeneo ya Mikoa ya Pwani ya kasikazini (Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Tanga na kisiwa cha Unguja) hadi tarehe 22 Disemba 2011. Mvua hizo zinatarajiwa kurejea katika hali ya kawaida kuanzia tarehe 23 Disemba katika maeneo hayo.
Aidha maeneo ya mikoa ya nyanda za juu kusini magharibi( Mikoa ya Mbeya, Iringa na Sumbawanga), kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida) na magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma na Tabora) yanatarajiwa kuendelea kuwa na mvua katika kiwango cha juu ya wastani pamoja na vipindi vya mvua kubwa. Hali hii inakwenda sambamba na utabiri wa mvua za Vuli na za Msimu ambapo maeneo mengi ya nchi yalitarajiwa kuwa na mvua juu ya wastani na vipindi vya mvua kubwa.
Kulingana na viwango vya mvua zilizonyesha katika kipindi kifupi ongezeko kidogo la mvua katika maeneo hayo linatarajiwa kuendelea kusababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu. Mamlaka inashauri tahadhari stahiki ziendelee kuzingatiwa.
Maeno mengine ya nchi yanatarajiwa kupata mvua za kawaida katika kipindi hicho. Aidha mwelekeo wa mvua katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari 2012 utatolewa mwishoni mwa mwezi huu.
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya Hali ya hewa na athari zake na itaendelea kutoa taarifa na tahadhari kila inapobidi.
Dk. Agnes L. Kijazi
MKURUGENZI MKUU
No comments:
Post a Comment