Tuesday, 1 November 2011

MH. ZITTO AFANYIWA UPASUAJI INDIA

 
MADAKTARI wa Hospitali ya Apollo iliyopo Bangalore, India kesho watamfanyia upasuaji Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe. 
Zitto alihamishiwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wiki iliyopita na baadaye kupelekwa India kwa matibabu zaidi ya maradhi ya kipanda uso ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa miaka 10 sasa. Watanzania Tumuombee.

1 comment:

Joel said...

Kwa uwezo wa Mungu atapona,ni m2 muhimu sana kwa maendeleo ya Tz
Tuzidi kumwombea dua njema