Sunday, 1 November 2015

Kijana wa miaka 7 amuudumia baba yake aliyepooza mwili

Kijana mwenye umri wa miaka saba anayeishi huko kusini magharibi mwa nchi ya china anaefahamika kwa jina la Ou Yanglin amekuwa akimuuguza baba yake mzazi "Ou Tangmin" aliyepooza mwili baada ya kuanguka ghorofani alipokuwa akifanyakazi ya ujenzi.
Mtoto huyo "Ou Yanglin" amekuwa akimuudumia mzazi huyo tangu mwaka jana "2014" baada ya kukumbwa na maradhi hayo. Amesema amekuwa akipata wakati mgumu kumuuguza baba yake baada ya mama yake mzazi kuondoka na wadogo zake wenye umri wa miaka mitatu na kutorudi tena nyumbani tangu mwaka jana.
Ou Yanglin amekuwa hapati muda wa dhiada kama watoto wenzie anaosoma nao baada ya kutoka shule yeye anakosa hata muda wa kucheza, kwani amekuwa akiangaika kumuandalia chakula baba yake na kutayarisha dawa kwa aajili ya kumpa mzazi wake.

Ou Yanglin huwa anaamka mapema alfajiri saa 12 asubuh na kumuandalia chakula baba yake kabla hajaenda shule na  kisha anarudi nyumbani mida ya mchana baada ya kula chakula cha mchana cha shule anarudi nyumbani kumuandalia baba yake chakula cha mchana na kisha kurudi shuleni kwa kuendelea na masomo na baada ya masomo anaomba fedha kwa baadhi ya watu na kununua dawa kwaajili ya baba yake.

Amesema anapata taabu sana kwakuwa yeye hana fedha za kumnunulia dawa baba yake na pia mazingira ya yeye kumuuguza pia imekuwa ni mtihani mkubwa sana kwake..hivyo anaomba kama kuna wa kumsaidia kwa hilo either kumpatia dawa au fedha za kununulia dawa.

Monday, 3 August 2015

Diamond anyakuwa tuzo nyingine

Msanii Diamond Platnumz sasa ni kama wiki kadhaa zimepita baada ya kutuwakirisha vyema kwenye tuzo za MTV-Africa (MTVMAMA) zilizofanyika nchini Africa ya kusini na kuweza kunyakua tuzo ya mtumbuizaji bora "best performer" 2015.... Jana ameweza kutuwakierisha tena ipasavyo kwa kutuletea tuzo ya msanii bora anaependwa Afrika na pia kwa wimbo bora unaopendwa Afrika "NANA"...Tuzo izo zijulikanazo kama "Hollywood and African people choice awards" ambazo zitatolewa 12 September.

Diamond ni miongoni mwa wasanii wanojituma sana na kuweza kuitumia sanaa kwa kutuwakirisha vyema Tanzania na Afrika mashariki vile vile Afrika kwa ujumla... 

Big Up sana mtu mzima Diamond Platnumz kwa hilo....

Sheria ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yaanza kazi

Mahakama ya kisutu jijini Dar es salaam yamepokea mashtaka kutoka kwa jeshi la polisi nchini baada ya kupata "maneno ya uchochezi" yaliyotolewa na kundi lililoundwa na watu wa kwenye mtandao wa kijamii (facebook), liitwalo "TANURU LA FIKRA".... Mashtaka hayo yamefunguliwa baada ya kuwepo kwa ujumbe wa mwanakikundi huyo ambaye anafahamika kwa jina la BRUNO COLMAN KIMARYOkwa yasemekana ni mkazi wa jiji la DSM kama ilivyoelezwa hapo juu kwenye picha inayoonesha "file la kesi"..... Ndugu Bruno aliandika maneno yanayoonesha uchochezi kwa kitendo kilichofanywa na majambazi waliovamia kituo cha polisi cha STAKI SHARI na kuwaua maaskari kadhaa na kuwapora bunduki....

Hii imeonesha sasa sheria dhidi ya maneno ya matusi, masengenyo, vitisho mbalimbali imeanza kufanyiwa kazi..... kwa wale watumiaji wa hii mitandao ya kijamii ningewaomba sana muwe makini maana wengi wenu mnaitumia sivyo.

Wednesday, 29 July 2015

Wachina wadakwa DSM wakifyatua maji feki

Wachina wakamatwa jijini Dar es salaam kwa kutengeneza maji pasipo kuwa na kibali cha kazi hiyo...wachina hao wanaoishi nchini kwa muda sasa wamedakwa na chupa mbalimbali za maji zikiwemo zenye nembo ya UHAI na Kilimanjaro na kujaza chupa hizo na kuzipeleka sokoni zikiwa na nembo hizo...ama kweli watanzania tunaishi kwa nguvu za Mungu tu!! Vitu feki vinaongezeka kila siku.

Tuesday, 28 July 2015

Picha: Lowasa akikabidhiwa kadi ya CHADEMA

Leo ndio ilikua siku ambayo takribani watanzania wengi wameshindwa kuamini kile alichokisema aliyekuwa waziri mkuu na pia mgombea urasi kwa tiketi ya chama cha mapinduzi, Mh. Edward Lowasa" pale alipotimiza yale aliyoahidi kipindi anatangaza nia ya kugombea urasi, kuwa endapo hatapitishwa kwenye nafasi ya kuwa mgombea basi atakihama chama hicho na kujiunga na chama pinzani....
Lowasa ametimiza hayo majira ya saa 10 jioni pale alipotangaza rasmi kukihama chama cha CCM na kujiunga na CHADEMA...

Picha baadhi zikionesha jinsi Lowasa alivyopokelewa na baadhi ya viongozi wa UkAWA na alivyokabidhiwa kadi ya CHADEMA.

Monday, 27 July 2015

Alichokisema Tundu Lisu kuhusu Lowasa kujiunga UKAWA

Tindu lisu ameandika haya katika ukurasa wake wa face book:

Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now. Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007. Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais. Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande. Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010. Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach. Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi. Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala. Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.

Kiumbe cha ajabu chadondoka Uingereza

Tukio Lisilo la Kawaida MALAIKA Aanguka Nchini UINGEREZA..Watu Wamiminika Kushuhudia Tukio lisilo la kawaida limetoa huko Uingereza....MALAIKA aanguka nchini UINGEREZA na kuifadhiwa sehemu maalum ambapo watu wameanza kumiminika kwenda kumshuhudia 

Lowasa akaribishwa UKAWA rasmi

Kikao cha Kamati Kuu cha dharura cha Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
kilifanyika jana Kunduchi Beach Hotel kuanzia
saa mbili hadi saa tisa usiku. Jumla ya
wajumbe 36 walihudhuria kikao hicho
akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu
Mkuu, Dr Wilbroad Slaa nk. Aidha, Edward
Lowasa alihudhuria kama mwalikwa ambapo
aligharamia mkutano huo ikiwa ni pamoja na
gharama za ukumbi, chakula, nauli na posho
za wajumbe. Kiasi cha fedha alichotoa
Lowasa ni milioni 500 ambazo zimetumika
kwa matumizi niliyoyataja hapo juu.
Katika kikao hicho, mjadala mkubwa ulitawala
juu ya ujio wa Edward Lowasa ndani ya
CHADEMA na hatimaye kupeperusha bendera
ya chama hicho. Kutokana na tishio alilotoa
Mwasisi wa CHADEMA, Edwin Mtei juu ya
kuwafukuza Slaa na Lissu ikiwa hawatakubali
Lowasa awe mgombea Urais, wajumbe hao
waliamua kuridhia kwa shingo upande
maamuzi ya wenye CHAMA. Kutokana na hali
hiyo, Wajumbe wote 36 kwa kauli moja
waliridhia Lowasa kujiunga na CHADEMA na
awe Mgombea Urais.
Taarifa hii inahitimisha minong'ono iliyotanda
siku nyingi tangu Lowasa akatwe. Kutokana
na maamuzi hayo, uongozi wa CHADEMA
umepanga kumtambulisha rasmi Lowasa
kesho Jumanne Julai 28 kwenye Hotel ya
Kilimanjaro Kempisk iliyopo Dar es Salaam.
Hata hivyo, ni lazima tujiulize kwa nini
Lowasa anautaka sana urais kwa udi na
uvumba? Je ni kweli ana uchungu wa kutatua
kero zinazowakabili wananchi? Kama ndo
hivyo, kwa nini akiwa Waziri Mkuu hakutumia
nafasi hiyo na badala yake alitumia kufanya
ufisadi hali iliyopelekea kujiuzulu kwake
kutokana na kashfa za Richmond?
Ni vema tukatambua Watanzania kuwa
Lowasa huyu huyu aliyekataliwa na Mwalimu
Nyerere ndiye anayejiunga na CHADEMA. Ni
Lowasa huyu huyu aliyekataliwa na CCM
ndiye anayejiunga CHADEMA. Ni Lowasa huyu
huyu aliyesimama kwa tambo nyingi akisema
kuwa atakuwa wa mwisho kuondoka CCM na
watakaomkataa waondoke wao ndiye
anayejiunga na CHADEMA.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyataja
mara kwa mara na kusisitiza kuwa ndiyo sifa
za Edward Ngoyai Lowasa kutofaa kuwa
kiongozi wa watu mambo yafuatayo;
1. Ni mtu mpenda mali na kujilimbikiza mali kwa
kiasi chochote na kwa hali yoyote
anayoiweza. Lowasa anamiliki mali ambazo
hazina maelezo ya jinsi alivyozipata. CCM
waliliona hilo na wakamfungashia virago.
2. Lowasa ni mtu dhaifu mbele ya mali na fedha
kwa sababu hiyo njia na nafasi yoyote iliyo
mbele yake anaweza kuitumia kupata fedha
zaidi na kujilimbukiza mali.
3. Ni mtu mwenye 'Pride' na kujitazama yeye tu
na kupenda kutambulika kwa mali aliyonayo.
Kwa sababu hiyo, anatumia muda na njia
nyingi kujijazia mali badala ya kuongoza na
kujali nchi yake (hii ndiyo sababu amekutwa
na kashfa lukuki za ufisadi na kubwa zaidi ni
ile ya Richmond iliyomfanya akaachia ngazi
nafasi ya Waziri Mkuu).
4. Lowasa anashindania zaidi kupata mali kwa
njia zozote, ziwe za halali ama haramu.
Kutokana na sababu hii ndio maana anajenga
chuki na kulipiza visasi kwa watu anaoona
kuwa vikwazo kwake katika kupata mali. Rejea
jinsi alivyotuhumiwa kushiriki kumtesa
Harrison Mwakyembe.
5. Lowasa huwajali zaidi matajiri kuliko watu wa
kipato cha chini. Hii ni kutokana na kulipa
fadhila kwa watu wanaomsaidia katika
harakati zake. Mathalan, wakati anatangaza
safari ya matumaini, Lowasa alikuwa
analazimisha wafanyabiashara kuchangia
harakati zake kwa ahadi ya kufanya biashara
na serikali akiwa Rais.
Kutokana na hoja hizi na nyingine nyingi bila
kusahau ugonjwa unaoendelea kumsulubu,
Lowasa hana sifa za hata kuteuliwa
kugombea Udiwani. CHADEMA wamehadaika
na tamaa ya fedha na wafuasi wa Lowasa.
Bilioni 10 alizohongwa Mbowe zimefanya
chama kitoke kwenye misingi yake na kuamua
kumpokea fisadi.
Nawahurumia sana Dr Slaa, Godbless Lema,
Tundu Lissu na wengineo ambao walijimaliza
kutaja madhaifu ya Lowasa akiwa CCM. Je
watafanya hivyo akiwa kwenye chama chao?
Tusubiri tuone.
Ila jambo moja tu napenda kuwahakikishia
wasomaji. Lowasa hana nafasi ya kushinda
Urais. Nasema haya kwa kujiamini.
Watanzania wamechoshwa na ufisadi.
Watanzania wamechoshwa na viongozi
wasiojali maslahi yao kama alivyo Lowasa.
Watanzania si wepesi wa kusahau.
Wameumizwa sana na hawa mafisadi na
mwaka 2015 ni wa kukata mizizi yote ya
ufisadi.

CHANZO: Mitandao ya kijamii

Tuesday, 24 March 2015

Diamond Platnumz aamua kumjibu Jux

Baada ya kupita siku kadhaa baada ya mkali wa Rn'b, Juma 'Jux' kutupia mjengo wake wenye ghorofa moja na kuuweka mtandaoni "Instagram"
...Mnyama "Diamond Platnumz" nayeye aamua kutupia mjengo wake wa hatari kwenye mtandao na kuonesha wadau kuwa habahatishi kwa kile anachokifanya..


Amazing Photoz