Wednesday, 11 December 2013

Demu wa kitambo wa Lil Wayne aionja jela

Aliyewahi kuwa demu wa mkali wa Hip Hop nchini Marekani mtu mzima Lil Wayne, mwanadadashosti Antonia Wright maarufu kama "Toya" amejikuta akichezeshwa lupango baada ya kuvunja masharti ya barabara. Toya alihamuliwa kusimamishwa na police wa usalama barabarani "Traffic" baada ya kuvunja sheria za barabara na kisha kudakwa katika sehemu ya kuegeshea magari katika "College" moja huko Georgia, Marekani usiku wa kuamkia jana (Dec 10).

Hata ivyo Toya aliamuliwa kutafutwa na kutiwa nguvuni kwa kuwa alikuwa na kesi nyingine ya kutoreport kituo cha polisi kwa kipindi cha nyuma. Kwa mujibu wa TMZ chombo husika kimeshindwa tolea maelezo ya kina kwanini Toya hakuweza fika polisi kama alivyotakiwa.

Toya aliachiwa asubuhi ya jana (Dec 11, Jumatano..saa 7:30) na kulazimika kutoa dhamana ya kiasi cha fedha $290. Baada ya kuachiwa aliungana na bwana ake wa kitambo (Lil Wayne) aliyekwenda kumuona huko lupango na kisha kusepa na mchizi wake ambaye ndiye mumewe wa ndoa "Mickey Wright"...kwa muji wa chanzo cha habari hii pia kimeripot kuwa mumewe "Mickey Wright" nae anakesi ya kudakwa na siraa katika uwanja wa Dege akiwa na mpango wa kuzisafirisha kinyume na sheria.


The Sporah Show yashinda tuzo ya kuwa kipindi bora cha "Out Standing Talk Show"

Kipindi maarufu cha "The Sporah Show" kinachofanywa na mwanadadashosti, Sporah Njau mwenye asili ya Kichaga kutoka nchini Tanzania mwenye makazi yake nchini Uingereza....ni moja ya vipindi vya "Out Standing Talk Show" kwa lugha ya kibongo "Kipindi cha mahojiano yanayofanywa kwa kusimama au kukaa chenye mazungumzo ya kawaida kuhusu maisha na mambo mengine ya kijamii" kilichopo huko Uingereza na kurushwa kupitia vituo mbalimbali vya luninga kama kwenye DSTV, GOTV na baadhi ya vituo vya luninga ambavyo ni maarufu, pia hupatikana kwenye mitandao kama "YouTube". Mara nyingi The Sporah Show huhoji mastaa na hata kwa wale ambao sio mastaa wa Afrika (Bongo) hususani wanaoenda UK au wanaoishi UK...

The Sporah Show imeweza kunyakua tuzo ya "THE OUT STANDING TALK SHOW" At The Tanzania Diaspora Achievement Awards In London At The Tanzania Convention, Trade and Investment Forum UK 2013.
Kwa kupitia ukurasa wake "The Sporah Show" wamepost picha ikimuonesha mwanadada Sporah akiwa na tuzo hiyo na kuandika maneno haya: