Tuesday, 12 November 2013

Belle 9:"Bado sijajua jina la wimbo wangu mpya"

Mbaka hivi sasa Belle 9 bado hajajua jina la wimbo wake mpya anaotarajia kuachia ndani ya mwezi huu (Novemba)...amesema hali hiyo ya kutojua jina la wimbo huo ni kutokana na maoni ya baadhi ya watu wake wa karibu waliopata nafasi ya kuusikiliza kutoa jina kwa mtazamo wao tofauti.

Kupitia mtandao wa facebook, mkali huyo toka Moro-Town amesema..."Mambo niaje watu wangu Wengi wanataka kujua jina la ngoma mpya kiukweli bado hatujapata jina rasmi maana tukiwa tunaiskiza kila mtu anataja jina lake ila mpaka jumatatu tutakua na jina Rasmi la ngoma yetu mpya asanteni na siku njema"

No comments:

Post a Comment