Saturday, 5 October 2013

Hatimaye AY amkumbuka Complex

Mkali wa commercial style, Ambwene Yessaya maarufu kama AY, leo kupitia mtandao wa instagram amepost picha yao wakiwa yeye, Adili Hisabati na marehemu complex...katika post hito AY ameambatanisha status yenye kubeba ujumbe wa kumkumbuka aliyekuwa producer wake kwa kipindi hicho anaanza game ya muziki, naweza sema Complex ni mmoja wa watu waliokuwa karibu sana na AY.

Simoni Sayi, maarufu kama Complex alifariki dunia mnamo mwaka 2005 kwa ajali ya gari akitokea Morogoro kuelekea mkoani Tanga wakiwa na kipenzi chake Vivian. Complex amefanya kazi nyingi sana na baadhi ya wasanii waliowika kitambo hiyo kwa kushirikiana nao ama kwa kuwatengenezea beats/midundo akiwa kama producer.

No comments:

Post a Comment