Wednesday, 3 April 2013

Wolper amuenzi kanumba kwa namna yake

Jacqueline Wolper Masawe au Wolpergambe kama anavyojiita mwenyewe katika mtamdao wa instagram, juzi kupitia mtandao huo wa instagram Jacqueline Wolper aliiambia jamii kuwa ameamua kumkumbuka aliyekuwa nguli kwenye tasnia ya filamu nchini, marehemu Steven Charles Kanumba kwa kuizindua filamu yake mpya aliyoi'direct yeye katika viwanja vya Leaders - DSM siku ya kumbukumbu ya marehemu Kanumba tarehe 07-04, ambapo itazinduliwa pia filamu mpya aliyoicheza marehemu kanumba mara ya mwisho inayoitwa "LOVE & POWER".

Siku hiyo ambayo itaudhuriwa na wadau mbalimbali wa filamu, celebrity mbalimbali pia viongozi mbalimbali watakuwepo katika viwanja vya Leaders katika kuazimisha siku hiyo,,,,wadau wote wa bongo movie mnakaribishwa katika viwanja vya Leadrs Club kiingilio ni BUREE.

No comments:

Post a Comment