Wednesday, 24 April 2013

Linex atimiza ndoto yake

Msanii Linex leo hii amekamilisha ndoto yake ya siku nyingi
kufanya kazi na msanii maarufu kutoka Kenya "Wyre", 
ngoma hiyo ambayo kwa msaada wa  digitali inaelekea 
kukamilika, imetengenezwa beat na producer Fundi 
Samweli ambae yupo Sweden kwa hivi sasa, ambayo 
ilitumwa kwa Linex na kuipeleka kwa producer Mswaki 
ambae pia ameongezea  maujuzi yake, na hapo 
ndipo linex akaingiza sauti zake.

Leo beat na vocal za Linex zimetumwa Kenya kwa ajili ya 
Wyre kuingiza sauti leo usiku na kisha 
kuongezea maujuzi pia akiwa kama producer..
kuonyesha furaha ya kukamilisha asilimia kubwa
ya kazi hiyo Linex ameamua kushare na mashabiki
zake kupitia ukurasa wake wa facebook kwa kuandika status hii

Linex Sunday:
"Siku ya leo imekua nzuri sana kwangu nimepiga kazi na mtu nnaemzimiaga kitambo linex ft wyre cumn soon but sita ahidi ni lini itatoka but saiz ndo kazi imeisha God is good"

SOURCE: this is diamond.com

No comments:

Post a Comment