Wednesday, 24 April 2013

Drake atoa msaada kwa muathirika wa kansa


Drake 
 Mwanamama huyo (Michelle)
Rap Drake Drizzy amejikuta anamsaidia mwanamama asiyemjua baada ya kumkuta katika mazingira magumu. Msanii huyo wa kimarekani, Drake jumapili iliyopita amejikuta akimsaidia mwanamama aliyejulikana kwa jina la Michelle aliyemkuta amejikunyata mtaani huko kusini mwa jiji la Las Angels nchini Marekani huku akiwa katika hali ya uzuni kwa kuwa hakuwa na mahali pakuishi, wala hajui atakula nini pia cha kusikitisha zaidi ni muathirika wa ugonjwa wa kansa.

Hivyo basi Drake akaamua kumpeleka mwanamama huyo katika hotel ya kifahari na kumlipia bili ya chakula kwa miezi mitatu na kumkabidhi kiasi cha fedha US$20,000 sawa na  Tshs 32,400,000. Drake na team yake wameahidi kumtafutia kazi mwanamama huyo na watakuwa wakimjulia hali kila wiki kutokana na ugonjwa huo unaomsumbua mwanamama Michelle.

"TONAOMBA RADHI KWA KUICHELEWESHA HABARI HII"

No comments:

Post a Comment