Sunday, 26 August 2012

dent wa chuo kikuu Nairobi awaambukiza hiv wanaume 322

Mtandao wa Daily Post umeandika kuwa mapema wiki hii kuna mtu wao wa karibu alipokea ujumbe wa simu kutoka kwa mwanafunzi wa kike wa chuo kikuu maarufu jijini Nairobi uliosomeka.

“Mimi ni mwanafunzi na nimeathirika na HIV. Niliapa kuusambaza  kwasababu niliambukizwa wakati wa tendo langu la kwanza. Nimeshatembea na wanaume 322 kwenye campus yangu na wawili nje. Nilitaka kuwaambukiza watu 2,500 lakini hatia niliyonayo inaniua.”

Ripoti hiyo ya kushtua imekuja miezi miwili tu baada ya mwanafunzi mwingine wa kike wa Moi University kuandika orodha ya majina 90 ya wanaume na kuibandika kwenye ubao wa matangazo wa chuoni hapo akidai kuwaambukiza (ama alijaribu kuwaambukiza makusudi) wote na virusi hivyo.

Kwenye orodha hiyo yalikuwemo majina mawili ya wanasiasa maarufu nchini Kenya.

Msichana huyo ana hasira kwasababu naye pia aliambukizwa ngoma siku ya kwanza ya kufanya mapenzi.

No comments:

Post a Comment