Friday, 20 April 2012

WIKI MBILI BAADA YA KIFO CHA KANUMBA

Wiki mbili kupita baada ya kifo cha aliyekuwa nguli katika tasnia ya filamu nchini, marehemu Steven Kanumba yaibuka mengi sana. Mbali na yanayoendelea kama kukisiwa kwa walioshiriki juu ya kifo chake, pia kuna moja limeibuka na kuwaacha watu midomo wazi pale mwanadada anayejulikana kwa jina la SALMA Hamidu, mkazi wa Igogo, jijini Mwanza ameibuka na kudai amezaa na marehemu Steven Kanumba mtoto wa kike aitwaye Treasure Steven Charles Kanumba (mwenye umri wa miaka 2), 

Akizungumza na mwandishi wa gazeti la Ijumaa, Salma anayefanya kazi kwenye Ofisi ya Uwakili ya Law Consultancy jijini Mwanza, alidai alianza kufahamiana na marehemu mwaka 2006 wakati yeye akiwa kwenye Kundi la Nyakato Arts chini ya Mwalimu Joseph.
CHANZO CHA UHUSIANO

Salma akasema kuwa, uhusiano wao uliunganishwa na Mwalimu Joseph ambaye alimpa marehemu namba zake za simu wakati alipopeleka filamu za Machozi Yangu na Siri Yangu kuifanyia uhariri (editing) jijini Dar es Salaam katika studio alizokuwa akifanyia kazi marehemu.

Amesema mashahidi wanaojua mkasa huo ni rafiki wa karibu wa marehemu aliwataja akiwemo na Swebe.
Mimi na wewe mdau hatujui wala hatuna kipingamizi wala kukubali swala hili, endelea kufuatilia blog hii kwa lolote litalothibitisha kuwa habari hizi ni za kweli basi mtataarifiwa..

No comments:

Post a Comment