Friday, 20 April 2012

KUNANI BONGO MOVIE??

SAJUKI
Wiki mbili sasa kupita tangu chama cha wacheza filamu nchini(BONGO MOVIE) kupatwa na majonzi ya kumpoteza mwenzao aliyekuwa nguli katika tasnia hiyo ya filamu marehemu Steven Kanumba, sasa wamekutwa na tatizo lingine la mmoja wa chama hicho bwana Sadick Juma Kilowoko alimaarufu kama Sajuki hali yake kiafya kuzidi kuwa mbaya. Sajuki alianza kuumwa au kusumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni(Tezi) mwanzoni mwa mwezi Novemba na kutibiwa katika Hospitali ya TMJ iliopo jijni Dar es salaam. Kwasasa hali ya msanii huyo imezidi kuwa hatarishi na kufanya apungue mwili na afya kuwa dhoofu.
Sajuki ambaye alipata pigo kubwa sana mwaka 2009 baada ya mkewe anayejulikana kwa jina la Wastara kupata ajali na kukatwa mguu.

Kwa mujibu wa mkewe Wastara, Sajuki alipokwenda katika Hospitali ya Apollo nchini India hivi karibuni alipewa dawa za kutumia kwa muda ambapo mwezi ujao (Mei) alitakiwa kurejea tena nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi.

CHAMA CHA BONGO MOVIE KINAOMBA MAOMBI YENU NA MSAADA WOWOTE ULE HATA KIFEDHA KATIKA KUMSAIDIA NDUGU YETU, JAMAA YETU BWANA SAJUKI.

No comments:

Post a Comment