Wednesday, 18 April 2012

USIYOYAJUA KUHUSU MWNAHARAKATI SHY-ROSE BHANJI

Kwa jina anaitwa Shy-Rose Bhanji, alimaarufu kama Mwanaharakati wa ukweli. Nimchanganyiko wa Kihindi na Kiafrika (Halfcast), yaani baba ni Mhindi na mama ni Muafrika. Kama anavyoeleza yeye mwenyewe kwenye 'profile' ya facebook, alipoteza wazazi wote akiwa mdogo sana.
Kuhusu maisha ya mahusiano siri yake hivyo siyajui na sina ruhusa ya kuyaweka bayana. Kwa kifupi Shy-Rose ni mkazi wa jiji la Dar-es-salaam, ni mtu mwenye upendo wa dhati kwa wanajamii pia ni mpiganaji wa ukweli kama anavyojiita mwenyewe (Mwanaharakati). Ni mwajiliwa wa NMB pia ni mmoja wa wabunge waliochaguliwa kuwa wabunge wa Afrika Mashariki. Dini ni 'Ismaili Muslim' na ni mwanachama wa chama cha mapinduzi (CCM).
Shy-Rose kiukweli ni mtu mwenye kupenda maendeleo na ni mtu mwenye kupenda challenge mbalimbali ambazo zinamlenga yeye au jamii kuifikisha hatua ya mbali.
HIZI NI BAADHI YA PICHA ZIKIJARIBU KUONESHA MAISHA YAKE NA JAMII HUSIKA
 Akicheza ngoma na wakazi wa Dodoma
 Hapa Simanjiro akiwapa taff wamasai
 Zanzibar akiwa na wakinamama
 Shy kwa wazee tu, hajambo. Hapa akipiga nao 
soga za hapa na pale huku wakifurahi pamoja
Hapa alikuwa njiani akielekea Kilosa
akapumzika na kukutana na huyu
mzee na kupiga story mbili tatu
 Alipotembelea Rorya Mission Hospital
 Siku ya wakinamama (Happy mother's day)alipotembelea moja
ya hospitali kwenda kuwaona nakuwafariji wazazi
Akiwa na watoto wilayani Njombe
Huwa kama mjinga akiwa social kwa watu
Akiwa na wakazi wa Kibaigwa
Bagamoyo na wanafunzi
Akiwa njiani kuelekea Kasulu alitua mahala kupata
ugali wa muhogo(Mzyenge)
Aki'show love na marehemu Steven Kanumba
kwenye moja ya party nyumbani kwake
KWA KIFUPI MWANADADA SHY-ROSE NI MTU MWENYE UPENDO NA KUJALI JAMII ZIMA KWA UJUMLA, SI KWA WANAWAKE WALA WANAUME, SI KWA RIKA WALA UMBILE. HAKIKA MUNGU AKUZIDISHIE UPENDO NA UKARIMU ULIONAO. PIA TUNAKUTAKIA MAFANIKIO MEMA KATIKA MAISHA YAKO YOTE NA KILA LA KHERI KATIKA KULITUMIKIA TAIFA LA TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA!!

No comments:

Post a Comment