Saturday, 14 April 2012

DIAMOND ANG'ARA TENA TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS

Diamond asumbua tena kwenye tuzo zinazotolewa kila mwaka kwa wasanii wa Musiki wa hapa Tanzania kupitia bia ya kilimanjaro, Tuzo hizo zijulikanazo kama Tanzania Kili Music Awards zinazohususisha vipengere tofauti vya musiki vikiwemo Taarabu, Bongo fleva, Musiki wa pwani yaani mduara, Reggae, na aina mbali mbali zitokanazo na midundo ya hapa bongo. Tuzo hizi zinatokana na jopo la upigaji kura toka kwa watanzania wenyewe kumchagua msanii wa nae mtaka kwa kipengere husika, hivyo Diamondi ameongoza kwa mara ya pili baada ya ile iliyofanyika mwaka juzi(2010) na kushinda vipengere vitatu (msanii bora wa anayechipukia, wimbo bora wa RnB na pia alichukua wimbo bora wa mwaka kwa kupitia wimbo wa Mbagala). Mbali na Diamond, pia kuna wasanii waliowika kama Suma Lee na Ommy Dimpoz wamechukua tuzo mbili mbili.
Pia wasanii waliteuliwa kuingia kwenye vipengere vingi na kutobahatika kupata tuzo ni Belle 9 ambaye kaweza kuingia kwenye vipengere vitatu (nyimbo bora ya RnB kwa kupitia Nilipe nisepe, mtunzi bora wa mwaka na pia mwimbaji bora wa kiume), Mzee yusuph pia amebahatika kuingia kwenye vipengere vingi lakini hakubahatika kupata Tuzo.
HII NDIO LIST YA WASANII WALIOPATA TUZO NA VIPENGERE VYAKE: 
1. WIMBO BORA WA RAGGAE 
ARUSHA GOLD BY WARRIORS FROM EAST
2. WIMBO BORA WA DANCE HALL. 
MANENO MANENO BY QUEEN DARLIN.
3. WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA.
DUSHELELE BY ALI KIBA.

4.BORA WENYE VIONJO VYA KIASILI.
VIFUU UTUNDU BY A.T

5. WIMBO BORA WA TAARABU.
NANI KAMA MAMA BY AISHA MASHAUZI.
6. WIMBO BORA WA KISWAHILI.
DUNIA DARAJA BY TWANGA PEPETA-
7. WIMBO BORA WA AFRO POP
HAKUNAGA BY SUMA LEE
8. WIMBO BORA WA R&B
NUMBER ONE FAN BY BEN PAUL
9. WIMBO BORA WA HIP HOP
MATHEMATICS BY ROMA
10. MSANII BORA ANAECHIPUKIA.
OMMY DIMPOZ

11. RAPA BORA WA BAND.
KALIJO KITOKOLOLO
12. MSANII BORA WA HIP HOP.
  ROMA MKATOLIKI
13. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA.
  NAI NAI BY OMMY DIMPOZ FT. ALI KIBA
14. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI.
KIGEUGEU BY JAGUAR
15. MTUMBWIZAJI BORA WA KIKE.
  KHADIJA KOPA
16. MTUMBWIZAJI BORA WA KIUME
DIAMOND
17. MTUNZI BORA WA MWAKA.
    DIAMOND

18. MTAYARISHAJI BORA WA  MUZIKI.
MANEKE
19. VIDEO BORA YA MWAKA.
MOYO WANGU BY DIAMOND

20. WIMBO BORA WA MWAKA.
HAKUNAGA BY SUMA LEE
21. HALL OF FAME.
     TAASISI JKT
22. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
      KING KIKII
23. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
     DR. REMMY ONGALA
24. MWIMBAJI BORA WA KIKE.
      LADY JAY DEE
25. MWIMBAJI BORA WA KIUME.
       BARNABA
 Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake 
kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro
 mara baada ya kutangazwa mshindi wa utuzi bora wa 
nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki 
bora za Kilimanjaro Music Award 2012 zilizofanyika usiku 
wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini 
Dar es salaam na kuhudhuria na wadau wa muziki 
kutoka ndani ya Tanzania  na nje ya nchi, 
Diamond amejipatia tuzo tatu kwa mpigo.
  Diamond  na wenzake kabla ya kuimba wimbo wa 
msondo akiwa na Ommy Dimpoz na Khalid Chokoraa 
wa bendi ya mapacha watatu.
 Msanii HBaba akiwa amezungukwa na vimwana
  P. Funk akiwa na msanii wa muziki wa Hiphop Jay Moo
 Wakurugenzi wa ASET kutoka kulia ni Asha Baraka 
akiwa na kaka yake Baraka pamoja na mdau mwingine 
katika hafla hiyo.
Dina Marios akiwa na Asma Makau
 Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey 
Nyange Kaburu kulia akibadilishana mawazo na 
Mulamu  Ghambi katika hafla hiyo.
Profesa Jay na Mkubwa Fella meneja wa kundi la 
TMK Family wakimkabidhi tuzo Roma akiwa 
Msanii wa muziki wa Hiphop aliyejishindia tuzo hiyo
Dyna akitumbuiza kwenye afla hiyo
  Recho akiwasha moto 
KWA MATUKIO ZAIDI NA PICHA JUU YA YALIYOJILI KWENYE TUZO HIZO 
CLICK HAPA KILI TUZO

No comments:

Post a Comment