Monday 18 August 2014

Hii inapendeza:Baadhi ya wasanii wajitokeza kumpa pole Afande Selle

Hii inapendeza sana hasa kuungana mkono kwenye vipindi vyote viwili "shida/matatizo na raha"....Natumaini wengi wenu mnafahamu kilichomkuta msanii mkongwe kwenye muziki wetu wa bongo fleva (Afande Selle) kwa kumpoteza mzazi mwenzie "Asha" maarufu kama "mama Tunda". Hivyo pasi mbali na kupokea salamu za rambirambi kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki zake wa karibu Afande Selle hususani wasanii wengine, pia kuna baadhi ya wasanii wameonesha moyo wa upendo kwa kuweza kufika na kumpa pole mwenzao huko mkoani Morogoro... Kama wengi tuliona baaadhi ya picha za matukio ya msibani, basi tulibahatika kumuona Professor Jay ambaye yeye alikuja na kuweza kuwahi shughuli nzima za mazishi... Pia kuna kundi la wasanii liliweza kuja japo lilichelewa shughuli za mazishi lakini liliweza kumpa pole mwenzao baada ya kupitia wakitoka kwenye ziara ya Kilimanjaro "Kili Tour".

Baadhi ya wasanii hao walikuwepo; Izzo Business, Ben Pol, Rich Mavocco, Joh Makini na bibie Malkia wa Taarabu nchi "mamaa Khadija Omary Khopa" na wengine ambao hawakuweza kuonekana kwenye picha na wapo walioshindwa kutambulika majina yao.
 Mamaa Khadija Kopa akimpa pole Afande
 Rapa kutoka Mbeya City "Izzo B" akimpa pole Afande

No comments: