Friday 25 July 2014

Rais JK amuahidi mlemavu bajaj

Ni moja ya tukio lililotawala kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii na vyomba mbalimbali vya habari, pale Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na mmoja wa wakazi wa kijiji cha Namtumbo mkoani Ruvuma wakati akiwa kwenye ziara mkoani humo. Mkazi huyo bwana Edwin Nganyani ambaye ni mremavu wa miguu yote kutokana na ajali aliyoipata ya kuungua na moto mnamo mwaka 2000. Mkazi huyo Edwin alimuomba msaada mh. rais na ndipo rais akamuahidi kijana huyo kuwa atahakikisha anampatia Bajaj ili iweze kumsaidia na kumrahisishia mazingira yake kuwa rahisi.

CHANZO: THE CITIZEN

No comments:

Post a Comment