Thursday 22 May 2014

Mtoto aliyeishi kwenye box miaka3

Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu na nusu, amekutwa akiwa mzima kwenye box yasemekana amekuwa akiishi humu kwa takribani ya miaka mitatu pasipo kuonekana na mtu yeyote yule.

Kitendo hicho cha kushangaza ambacho kimefananishwa na kitendo cha kimazingara kimetokea kata ya Kiwanja cha ndege mkoani Morogoro juzi (Mei 20), ambapo amtoto huyo aliyeachwa na mama yake mzazi (marehemu) na kulelewa na mama mdogo amekutwa akiwa kwenye box na majirani waliojitolea kwenda kutoa taarifa katika kituo cha polisi kilichopo jirani na mitaa hiyo.

Kwa mujibu wa majirani wamedai kuwa mtoto huyo alikuwa akisikika akilia nyakati za asubuhi na usiku, lakini cha kushangaza hawakuweza kumuona mtoto huyo wala kufahamu anakofichwa katika chumba cha mama huyo ambaye ni mama mlezi wa mtoto huyo. Kwa mujibu wa baba yake mzazi mtoto huyo amesema binafsi hajui kwanini akuweza kuoneshwa mtoto wake pindi anapokuja kuwatembelea na kuacha pesa ya matumizi kwa mtoto huyo zaidi ya kuambiwa amelala na kuacha pesa na kuondoka pasipo kuwa na fikira yeyote kuhusiana na majibu hayo aliyokuwa akipatiwa na mama mlezi huyo ambaye ni shemeji yake. Pia baba amesema ameshindwa kufahamu ni kwanini amtoto amekuwa akilishwa pumba kwa kipindi chote hicho ingawaje amekuwa akiwapelekea pesa za matumizi kila mwisho wa mwezi upeleka laki moja kama pesa ya matumizi kwa mtoto wake.

Afya ya mtoto huyo si ya kuridhisha sana kwani ni mlemavu tangu alipozaliwa na kuachwa na mama yake, na sasa imezidi kuwa mbaya kutokana na kukosa lishe nzuri.

Kesi bado ipo mikononi mwa polisi na mbaka sasa mama huyo mlezi yuko mikononi mwa polisi kwa madai ya malezi yenye mazingira ya kutatanisha kwa mtoto huyo.

No comments:

Post a Comment