Tuesday 6 May 2014

Chris asherehekea b'day yake jela

Mkali wa muziki wa Rn'B kutoka nchini Marekani "Chris Brown", amejikuta akisherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake akiwa jela...hii ilimshangaza zaidi baada ya kufikishwa mahakamani siku ya Alhamis na kesi yake kusogezwa mbele (wiki mbili), ndipo hapo alipojikuta akisherehekea siku ya kuzaliwa kwake (Mei 5) akiwa jela.

Mwanamuziki huyo anakabiliwa na kesi ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake, mwanamuziki mwenzie "Rihanna"... anatarajia kupandishwa tena kizimbani May 09. Ambapo kesi yake nyingine ilipangwa kusikilizwa jana (May 06). Pia Chris Brown anakabiliwa na kesi ya kutaka kupigana nje ya hotel iliyopo huko Washington DC, Marekani mnamo mwaka jana...kesi hiyo ambayo inasemekana kama atakutwa na hatia basi atachezea kifungo cha miezi 6 jela.

No comments: