Monday 13 January 2014

Dogo abahatika ku'rap na Jigga kwenye jukwaa moja

Ni miongoni mwa vitendo vinavyofanya mara chache sana tena na wasanii walio wachache sana wenye mafanikio kuwapa moyo/motisha wasanii wachanga au baadhi ya watu wenye ndoto za kuwa wasanii na kuweza kutimiza ndoto zao za kuwa big star. Kitendo hiki kimefanywa na big star from US, Jay Z akiwa kwenye concert yake ya "Magna Carter Holy Grail" huko Chicago nchini Marekani.

Baada ya kumchagua dogo mwenye umri wa miaka 12 akiwa kwenye concert yake mwanzoni wa wiki iliyopita huko New York City, Marekani....Jay Z pia amefanya hivyo kwa kuweza kumchagua underground mwingine mwenye ndoto za kuwa bigstar mwenye umri wa miaka 19 kwenye tamasha lake huko Chicago. Underground huyo ambaye ni binti aliyefahamika kwa jina la Monique Burrell na jina la usanii "MoBo The Great, aliwezakuonesha kipaji chake kwa kupanda stage moja na mkali huyo.

Kwa mujibu wa chanzo cha story hii kinasema Jay Z alimchagua mtoto huyo toka kwenye umati wa watu waliokuwepo kwenye concert hiyo na kuweza kumpa nafasi ya kuperform na kupata nafasi ya kusikilizwa na crowd ya watu waliohudhuria tamasha hilo.

Story zinasema kuwa baada ya binti huyo kupanda on stage alipokamata kipaza sauti tu, alimueleza mtu mzima Jay Z kuwa kama alishawahi kurap wakati dogo akiwa na umri wa miaka 16 kwenye tour ya concert yake ya Blueprint 3 na sasa ana miaka 19 na yupo tayari. "I was 16 when I rapped on stage with you for BP3. I'm 19 and READY!

Baada ya dogo kuperform, Jay Z na ulinzi wake wakamfuata binti huyo na kuweza kuzungumza nae...Jay Z amesema anaahidi kuwa atafanya kila jitihada dogo aweze timiza ndoto zake na atakuwa akiperform kila anapopata nafasi.

ITAZAME VIDEO HIYO HAPA

No comments: