Tuesday 10 December 2013

Mazishi ya Mandela yawakutanisha viongozi wa mataifa mbalimbali

Barack Obama na Raul Castro wa Cuba
RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela, mweusi wa kwanza kushika wadhifa huo katika taifa lenye uwezo mkubwa kiuchumi na kijeshi barani Afrika, alifariki dunia Alhamisi iliyopita akiwa nyumbani kwake jijini Johannesburg.

Leo imefanyika ibada kubwa ya kitaifa Uwanja wa FNB, Johannesburg kumuaga Nelson Mandela ambapo viongozi mbalimbali watahudhuria ibada hiyo wakiwemo Rais Barrack Obama na mkewe Michelle, Rais Jakaya Kikwete, Rais Robert Mugabe na mkewe, Rais Uhuru Kenyatta na mkewe, Rais Yoweri Museveni, Rais Joyce Banda na wengineo wengi

Kifo chake kimeushtua ulimwengu na kwa mara ya kwanza katika historia, dunia nzima imesimama nyuma ya Kiongozi huyo, kila mmoja akionesha masikitiko yake.

Wakati dunia ikisubiri mazishi yake ambayo yanatarajiwa kuvunja rekodi ya mazishi yote yaliyowahi kufanywa tokea kuumbwa kwa uso wa dunia hapo Desemba 15 mwaka huu.

Katika mazishi hayo yanayotarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali Duniani kama kiongozi mkuu wa Madhehebu ya Romani,Papa Benedict XVI,Rais Obama mwenyewe na mkewe Michelle, George Bush na mkewe Laura, Bill Clinton na mkewe Hillary, Rais wa 39 wa Marekani, Jimmy Carter naye atakuwepo ila baba yake George W. Bush, George Bush senior huenda asiende kutokana na urefu wa safari hiyo.

Upande wa Marekani katika kumuenzi Mzee Nelson Mandela,Jengo moja la serikali jijini New York, Marekani limebadilishwa taa za kulipamba jengo hilo na kuonesha bendera ya taifa la Afrika Kusini...

No comments:

Post a Comment