Thursday 26 September 2013

Ujumbe kutoka kwa R.O.M.A

Ni ndefu ila ukipata nafasi SOMA!!

"WANAOFANIKIWA KIMAISHA"

Wakishatoka kimaisha, hata kama sio kwa kiwango kikubwa!! wanawasahau waliokuwa nao kipindi wanatafuta hayo mafanikio!! wanawasahau WAPENZI wao/ MARAFIKI zao/hata NDUGU zao wakati mwingine!! na sio tu kuwasahau!! WANAWAKATAA NA KUWATUPA WAKATI MWINGINE(KUWAPOTEZEA)!!

Wanapata marafiki/wapenzi wapya ambao kimsingi kabisa wanakuwa wamejuana nao kwasababu tu wameshakuwa watu fulani ktk maisha!! 
pengine wapenzi na marafiki hao wapya hata wasingekubali kukaa karibu naye kipindi kile anatafuta!!
Hujawahi kuona mtu ana-spend na marafiki ambao wamekutana tu mjini na wapo naye kwasababu tu yeye ni mtu fulani!! 
na wakati huo huo jamaa huyo ana dada yake/mdogo wake yupo nyumbani/kijijini anahitaji sh. 1000/= akashone shati la shule tuu!! 
NA ATAMNYIMA PESA HIYO NDOGO/ ILA ATANUNULIA MAKAHABA POMBE BAR!!
Sawa sio mbaya kuwa na marafiki wapya, na pengine hao marafiki ndio wamempa maisha hayo bora!! 
lakini ni jambo la kutafakari sana........UKIFA HUJUI NANI ATAOSHA MAITI YAKO/ HUJUI NANI ATASAFIRISHA MWILI WAKO NA KUKUZIKA NA KUKUSITIRI KWA YOTE!! SIO MARAFIKI NA WAPENZI WOOTE WATAKAOKUWA NAWE KWENYE SHIDA!!

Tambua wewe umemaliza chuo na umebahatika kupata kazi fasta/ ila wapo wenzako tena waliokuwa wanakuongoza darasani, wapo tu street!!
"choka mbaya"!!
usiwatupe sana!! 
timiza ahadi mlizopeana kipindi mnahaso kumtafuta elimu kwenye VIMBWETA!!!.....wewe umetangulia tu kubahatika!!

BADILIKA!!

"WASIOFANIKIWA/AMBAO BADO WANATAFUTA"

Mara nyigi ukiwa na shida, basi kila ambaye hatakusaidia utamuona ADUI kwako!! wengi hatukubali mabadiliko ya watu!!
tunapozidi kukua na majukumu yanazidi pia!!

Ndio tulipanga foleni wote ktk kutafuta, na leo nimebahatika kuanza kufanikiwa mimi!! isiwe kuwa mimi ndiyo niubebe msalaba wako wooote!!

Nikikutana nawewe pengine sitaweza kubadili maisha yako ktk kiwango chote/ pengine wewe unaona nina nafasi kubwa sana ya kukusaidia, kumbe la hasha!! siwezi kukusaidia kwa kiwango hicho!!

Basi aliyefanikiwa amerudi nyumbani na kuwakuta marafiki zake bado hawajayatoa maisha!!(HAWAJAGEMUA) basi ataenda nao outs na kuwapa bia nyingi na wataenjoy sana usiku huo!! na pengine asubuhi bia zikiisha watalaumu kuwa pesa ya bia bora ungetupa kama mtaji!!

hahahahhaha!! maisha bana!! sidhani kama kuna usahihi hapa!!! Nways.....

Unatamani uwatoe ktk dhiki ile, lakini huna uwezo huo kwa muda huo!! una familia kubwa na ya kwako pia/unataka uanze kujijenga/na kuwekeza kwa sana!! hujui uanze na nani umalize na kipi!!

NA KIPINDI HIKI NDICHO KINAPELEKEA UKATALIWE NA MARAFIKI WENGI WA ZAMANI, MAANA HUONA HAUNA MSAADA KWAO!! 
na hapa ndipo huanza lugha za-

A)JAMAA KACHANGE SANA......
B)MWANA KAWA SNITCH SAIVI....
C)DOGO KAIASI KAMBI....
D) TUTAONA MWISHO WAKE HAPA NDIO MTAKUJA VILLAGE.....
E) WALIKWEPO KINA FULANI BANA LEO WAKWAPI, VINA MWISHO....!!

ETC!!

Wasiofanikiwa watalaumu sana kama wanakupiga kizinga cha buku kumi aaaf unawambia huna!!
kisha baadae wanakukuta umekaa maeneo unakunywa na wana!!

Na mtu huyu atakulaumu sana kuwa hujamsaidia, ilhali pesa unazo, na pesa hizo unazifanyia mambo yasiyo na msingi!!(yeye ameona siyo ya msingi)!!

Kumbe pengine wewe ulishatoa sana pesa kwa watu wengine toka umepokea mshahara wako, hadi hiyo iliyobaki ukasema sasa hii ninywe pombe kama starehe kwa kazi nzito nianyayo!!
na pale pale ndio kizinga cha rafiki wa karibu kinatokea!!

Ndiyo maana kuna muda ulimuomba mama/baba pesa ndogo tu, akakujibu HANA!! sio kama kweli HANA!! NAKATAA!! NI MIPANGO NA MATUMIZI!!

Says Rooomaaa!!

UMEJIFUNZA NINI EWE RAFIKI!!??

1 comment: