Thursday 19 September 2013

Mdada amkata mwenzie na viwembe na kisha kuvuliwa nguo zote

Tukio hilo la kusikitisha limetokea siku mbili zilizopita huko Makurdi, mtaa wa Iniko nchini Nigeria, ambapo mdada alimcharanga mwenzie kwa viwembe katika sehemu za usoni baada ya malumbano yaliyodaiwa kusababishwa na kuchukuliana bwana.
Wadada hao walizozana kwa muda na kushindwa kufikia muhafaka kwa madai ya kuchukuliana bwana, ambapo yarepotiwa kuwa mshtakiwa (aliyemchana mwenziye na viwembe) ndiye alianza kutoka na bwana huyo waliomuita Sugar Daddy kwa kuwa alikuwa kama Buzz tu wakumchuna na kisha kwenda kumsimulia mwenzie, na mwenzie akachukua uamuzi wa kutembea na Sugar Daddy huyo...ndipo ugomvi ulipoanzia. Kwa mujibu wa habari kamili zimedai kuwa tukio hilo lililotokea jumanne ya wiki hii limechukua picha ya namna yake baada ya mdada huyo kumjeruhi mwenzie kwa viwembe sehemu za usoni kisha akatiwa nguvuni na kutolewa nguo zote na kuachwa kama alivyozaliwa.

No comments:

Post a Comment