Tuesday 10 September 2013

Binti aliyedai kuzaa na Diamond

Huyu ndiye binti wa kidato cha nne aliyeibuka na kusema kwamba amezaa na 'Diamond Platinum'

Baada ya kupata madai hayo, binti huyo Sasha mwanzo alisita kuzungumza lakini baadaye akakiri kuzalishwa na mwanamuziki huyo na kudai kuwa kwa kuwa hamjali tena, naye aliacha kumfuatilia.

Haya ndio maneno ya binti huyo kuhusu Diamond '“Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana miezi mitatu sasa. Unajua yeye ndiye alinikatisha masomo na kusema kuwa ataniendeleza na atamlea mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona tena sababu ya kumfuatilia kwa vile kwetu napata kila kitu,” alisema Sasha.

Baada ya taarifa hizo kuenea Diamond alipotafutwa alipewa nafasi ya kuzungumza juu ya sakata hili alisema hivi '“Hahahaaa…mbona hiyo ishu ni kubwa sana kwangu! Ukweli huyo mwanamke simjui kabisa. Lete stori nyingine achana na hiyo.” alisema Diamond...

No comments:

Post a Comment