Tuesday 20 August 2013

Video:Amber Rose akizungusha wenzele na gauni la harusi

Mke wa Rapa maarufu nchi marekani, Amber Rose mwenye umri wa miaka 29 amejikuta anapost video yake akicheza huku akiwa amevaa gauni la harusi yake na Rapa huyo (Wiz Khalifa). Mwanadada huyo alijiachia vya kutosha japo video ni fupi....

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 25, Wiz Khalifa ambaye ni mume wa mwanadada huyo mwanamitindo (Amber Rose) ameviambia baadhi ya vyombo vya habari kuwa yeye na Amber tayari wameshafunga ndoa mwezi mmoja uliopita, japo ni ndoa ya kiserikali (courthouse - wedding). Hata hivyo ni jambo ambalo Wiz amelitekeleza baada ya kile alichowahi kutamka mwezi Oktoba mwaka jana (2012) kupitia mahojiano aliyofanya na XXL magazine kuwa wameamua kuhairisha mipango yao ya ndoa kwa muda ule kwa sababu wanampango wa kupata mtoto na sio poa kufunga ndoa huku Amber akiwa mjamzito, so watasubiri mbaka wapate mtoto na ndipo wafunge ndoa...ila watafunga ndoa ya bomani au ndoa ya kiserikali (ya mahakama) kabla ya mtoto wao kuzaliwa na ndipo wafunge ndoa ya kawaida...."But we’ll probably get licensed and married before the baby’s born, and do a wedding afterwards because it makes more sense for the baby to be in the wedding than for her to be pregnant.  Some people, they rush and do it. But, it works both ways.”
Wiz na Amber sasa wanamtoto mmoja aliyezaliwa mwezi Feb 21, mwaka huu na kupewa jina la Sebastian.
ITAZAME VIDEO HIYO

No comments: