Friday 23 August 2013

Ndege yaanguka ziwa Manyara

Ndege aina ya Vich Grave (Pichani) yenye namba za usajili 5H/EPW mali ya TanzaAir ilipata hitilafu katika injini yake na kupelekea kuanguka katika Ziwa Manyara jana. Taarifa zilizopatikana kutoka kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, kutokana na hitilafu hiyo ya injini rubani wake aliyetambulika kwa jina moja la Kapteni Kondo (51) alilazimika kuishusha lakini ikaanguka kwenye ziwa hilo.

Katika ajali hiyo abiria wote sita waliokuwemo na rubani wamenusurika kufa ingawa walipata majeraha madogo madogo ambapo walikimbizwa hadi Hospitali ya Selian inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Kati kwa matibabu.

Aliwataja abiria hao kuwa ni Anik Kashasa (51), Regina Mtabihirwa(58), Aloyce Mwanga (60), Naburi Meeda (80), Ashura Mohamed (38)pamoja na Protas Ishengoma (45) wote wakazi wa jijini Dar es Salaam. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema ndege hiyo ilikuwa ikitokea Bukoba kwenda jijini Dar es Salaam kupitia Zanzibar.

CHANZO: Dar24.com

No comments: